Mapema leo nyota wa PSG na timu ya Taifa ya Ufaransa, Achraf Hakimi alishiriki hafla ya kutoa msaada kwa shule ya watoto wenye mahitaji maalumu ya Patandi Sekondari chini ya Taasisi ya taasisi yake kwa kushirikiana na GSM Foundation iliyowakilishwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said
Akizungumza katika hafla hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza kwake kufanya 'charity' nje ya Taifa lake Morocco, Hakimi ameeleza furaha yake kwa kushiriki tukio hilo huku akimshukuru Hersi kwa kufanikisha tukio hilo
"Nimefurahi kuwa nanyi na kutumia sehemu yangu ya likizo hapa Tanzania. Niliongea na kaka yangu Hersi tulipokutana Paris na amekuwa sehemu muhimu ya Safari yangu ya kuja Tanzania"
"Kutoka moyoni napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wote wanaofanya kazi kubwa ya kuwalea watoto hawa na ninaamini siku moja nitakuja tena kuwa pamoja nanyi," alisema Hakimi
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amemshukuru Hakimi kwa kuichagua Tanzania kuwa nchi yake ya kupumzika baada ya msimu wa mashindano akiwa na PSG
"Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Hakimi kuja Tanzania na mpaka sasa Hakimi ameshakaa siku tatu na kujionea vivutio vya utalii ndani ya Serengeti na Ngorongoro nashukuru kwa kuchagua kuja kwenye nchi yetu nzuri ya Tanzania"
"Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Hakimi kutoa msaada nje ya nchi yake ya Morocco na leo watoto wetu watapokea Kompyuta za kisasa, marekebisho na maeneo muhimu pamoja na vifaa vingine vingi na sisi kama Watanzania na hawa watoto wenye uhitaji tumefarijika sana kwa kupata mahitaji haya muhimu kwa watoto wetu"
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametenga muda wake pamoja na rasilimali zake kuueleza Ulimwengu namna nchi yetu ilivyobarikiwa Vivutio vya utalii na leo hii Hakimi yupo hapa Tanzania kwaajili ya kufanya utalii na sisi tulimuomba afanye chochote akiwa hapa kwakuwa amekua akirejesha kwa jamii mara kwa mara akiwa nchini kwao Morocco"
"Kwa asilimia mia moja alikubali ombi letu na leo hii tupo hapa kukamilisha," alisema Hersi