Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amekanusha tetesi zilizovuma mitandaoni juu ya Pacome Zouzoua kuomba kuondoka baada ya kupata ofa kutoka timu mbalimbali wakiwemo mabingwa wa Afrika, Al Ahly
Kamwe amesema mpaka sasa Yanga haijapokea ofa kutoka timu yoyote kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja
"Taarifa kuhusu Pacome ni uzushi tu ulioanzishwa na watu ambao wanatafuta faraja baada ya mambo yao kutokuwa mazuri"
"Pacome ni mchezaji wa Yanga na bado ana mkataba wa mwaka mmoja. Hatujapokea ofa yoyote kwa ajili yake"
"Niwaambie tu, uongozi tayari umeanza mchakato wa kumuongeza mkataba ambao utamuweka Jangwani kwa muda mrefu zaidi," alisema Kamwe
Yanga iko mbioni kumuongeza Pacome mkataba wa miaka miwili ambao utamfanya adumu Jangwani mpaka 2027