Wachezaji Yanga watakiwa Avic Town Jumatatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2024
Wachezaji Yanga watakiwa Avic Town Jumatatu

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanatarajia kuanza kuripoti Avic Town kesho Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa mwaka 2024/2025

Wito huo umetolewa na Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ambaye anatarajiwa kurejea nchini mapema wiki inayoanza kesho akitokeea Argentina alikokwenda kwa ajili ya mapumziko baada ya kumaliza msimu uliopita

Taarifa kutoka Yanga zinasema Gamondi amewataka wachezaji wote wapya na wale waliosalia katika kikosi hicho kuwapo jijini Dar es Salaam Julai Mosi

Chanzo hicho kimesema Gamondi ametuma ujumbe wa simu kwa viongozi, kuhakikisha wanamaliza mchakato wa usajili haraka huku akiwataka wachezaji wote kuripoti kambini kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuanza mawindo

"Kocha ametuma ujumbe, amesema bila kujali mchezaji mpya au wa zamani, pamoja na watu wa benchi la ufundi kila mmoja anatakiwa awe amewasili kambini Julai Mosi, kwa hiyo viongozi wameambiwa wamalize kila kitu kuhusu usajili ili akifika isiwe tena kuna mchezaji hajafika au kukamilisha usajili," kimesema chanzoΒ 

Naye Rais wa Yanga, Hersi Said, amesema klabu hiyo itaanza kutangaza nyota wapya waliosajiliwa na inaowatema kuanzia kesho. Hersi amesema usajili wa kikosi chao umeshakamilika na kinachosubiriwa ni kukabidhi majina katika Idara ya Habari ya klabu hiyo

"Tumeshasajili karibu asilima 99, kazi imekwisha, hivi sasa tumeiachia tu Idara ya Habari kutengeneza njia nzuri ya kutambulisha wachezaji, kuna maeneo ambayo tumelazimika kuyaboresha katika kikosi chetu ili kuwa bora zaidi, kwa hiyo nichukue fursa hii kuwaambia Wana-Yanga wawe tayari kuanzia tarehe moja tutaanza kutoa taarifa za usajili, wachezaji wetu wapya na wale tunaowaongezea mikataba na tutakaowaacha," Hersi amesema

Yanga inatarajia kuweka kambi yake Ulaya lakini imeweka wazi imepokea mwaliko wa kucheza mechi za kirafiki za kimataifa katika nchi za Kenya, Rwanda na Afrika Kusini

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’