Manji kuzikwa leo Marekani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jul 2024
Manji kuzikwa leo Marekani

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Yanga, Yusuf Manji anatarajiwa kuzikwa leo nchini Marekani. Manji alifariki usiku wa kuamkia jana katika hospitalini Florida huko Marekani 

Kwa mujibu wa taarifa ambayo mtoto wa marehemu Mehbub Manji ameitoa, familia wanashukuru kwa jinsi ambavyo Watanzania wameendelea kuombeleza kifo cha baba yao na jinsi ambavyo wameendelea kumuombea huko alipo.

"Tunawaomba muendelee kumuombea baba yetu awe na safari njema huko aendapo. Alikuwa anaipenda Tanzania na Watanzania wanampenda sana, lakini tunaomba kuwaambia kuwa Manji atazikwa leo saa tisa alasiri Orlando, Florida Marekani, karibu na sehemu aliyozikwa baba yake. Baba tulikupenda lakini Allah amekupenda zaidi. Yusuf Manji: Ni baba, rafiki, kiongozi," ilimalizia taarifa hiyo

Manji ambaye aliingia madarakani mwaka 2012, alikuwa Mwenyekiti wa Yanga kwa kipindi cha miaka mitano tangu mwaka 2012 hadi 2017 na kufanikiwa kutwaa makombe manne ya Ligi Kuu Bara, Kombe moja la FA, Ngao ya Jamii na Kombe la Kagame

Manji anatajwa kuwa mwekezaji wa kwanza kwenye soka la Tanzania kuongeza thamani za wachezaji ambapo katika kipindi cha uongozi wake, mishahara na 'signing fees' za wachezaji zilianza kupanda

Wachezaji kama Kelvin Yondani, Emmenuel Okwi, Juma Kaseja aliowasajili kutoka Simba, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Obrey Chirwa na hata Mrisho Ngasa wanaweza kuthibitisha ni kwa kiasi gani Manji alipandisha thamani zao

Manji alikuwa na upendo mkubwa kwa klabu ya Yanga, kauli yake ya mwisho aliposhiriki Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga 2022/23 alisema moyo wake ameuacha Yanga

Aliipenda na kuisaidia Yanga kila alipohitajika kufanya hivyo, mara kadhaa aliwalipia tiketi mashabiki wote wa Yanga na kushuhudia baadhi ya mechi bure

Kwa hakika Manji ataendelea kuishi katika mioyo ya Wanayanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’