Bado hatujamaliza kumtambulisha Chama - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2024
Bado hatujamaliza kumtambulisha Chama - Kamwe

Klabu ya Yanga imeandaa utaratibu maalum wa utambulisho wa kiungo mshambuliaji Clatous Chama aliyesajiliwa na mabingwa hao wa nchi kutoka klabu ya Simba

Imezoeleka Yanga hutambulisha wachezaji wake wapya kwa utaratibi tofauti na ule uliotumika hapo jana

Jambo hilo liliibua maswali miongoni mwa wadau na kupelekea baadhi ya watu kusambaza uzushi juu ya usajili huo

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kamwe alisema utambulisho waliofanya jana ni mwanzo tu, kwani wameandaa tukio maalum kumkaribisha Chama Jangwani

"Hatukufanya vile kwa kukurupuka tu, lazima ifahamike hii ni biashara ya mpira wa miguu. Unajua baada ya utambulisho ule ni kampuni ngapi zimeulizia kuhusu utambulisho rasmi wa mchezaji akiwa na jezi ya Yanga? Unajua ni kwa kiasi gani tumetengeza shauku ya watu kutaka kumuona Chama katika jezi ya Yanga?," alihoji Kamwe

"Suala la Usajili wa Chama ni sehemu ya biashara yetu. Kila mtu anakiri kuwa usajili wa Chama ni usajili mkubwa. Mtiririko wa matukio ya usajili huu wa Chama kwetu ni fursa. Najua wengi wanatamani kujua Chama ataonekanaje na jezi ya Yanga. Hapo ndipo tunalenga kuuza usajili huu," alisema

Kamwe amesema Yanga ndio klabu ya kwanza kuja na utaratibu wa kutambulisha wachezaji wapya kupitia video fupi fupi, Kila wakati watakuja na ubunifu tofauti lengo likiwa kuinufaisha klabu kutokana na usajili huo

Aidha Kamwe amedokeza leo jioni watatambulisha usajili wa mchezaji mwingine ambao nao wataufanya kwa utaratibu tofauti

Kamwe amezindua huduma ya Yanga Habari ambapo wanachama na mashabiki wataweza kupata habari muhimu za timu yao kupitia ujumbe mfupi (SMS)

Gharama za kupata Yanga Habari kwa wiki ni Tsh 500 na kwa mwezi Tsh 2000. Huduma hiyo inapatikana kwa kujiunga kupitia *149*40#

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’