Mpaka sasa Yanga imethibitisha kuwaongezea mikataba kiraka Farid Mussa na mlinda lango Djigui Diarra huku ikiachana na golikipa Metacha Mnata
Baada ya msimu uliopita kufika tamati na Yanga kutwaa ubingwa, pendekezo la kwanza la kocha Miguel Gamondi wakati wa mazungumzo ya kuhuisha mkataba wake lilikuwa kuhakikishiwa nyota muhimu wa kikosi chake wanaendelea kubaki
Yanga imepigana na kushinda vita ngumu dhidi ya miamba waliokuwa wakiwanyemelea mastaa waliofanya vizuri msimu uliopita
Makocha wana msemo wao kuwa usajili bora ni kubaki na wachezaji wako muhimu katika kikosi
Kwa maana wakati mwingine unaweza kusajili mchezaji mpya lakini akashindwa kufikia matarajio kutokana na changamoto mbalimbali
Yanga imefanikiwa kuwaongeza mikataba nyota kama Stephane Aziz Ki, Diarra, Bakari Mwamnyeto, Farid, Jonas Mkude, Khalid Aucho huku pia ikiendelea na zoezi la kurefusha mikataba ya nyota wengine kama Kennedy Musonda, Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua, Dickson Job na Yao Kouassi ambayo watakuwa wachezaji huru mwishoni mwa msimu ujao
Gamondi amebaki na asilimia 90 ya wachezaji aliokuwa nao msimu uliopita huku akiongezewa 'silaha' nyingine ili kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto
Msimu ujao Yanga haianzi upya kama watani zao Simba ambao kila siku wanatambulisha wachezaji, bali Wananchi wanakwenda kuendeleza pale walipoishia msimu uliopita