Hali ya hewa ya baridi katika mji wa Awassa imekuwa ikiwasumbua wachezaji wa Yanga ambao kesho wanashuka kwenye uwanja wa Hawassa kuikabili Wolaitta Dicha.
Meneja wa Yanga Hafidhi Saleh amesema imekuwa jambo jema kwao kufika mapema kwenye mji huo na anategemea wachezaji wataizoea hali ya hewa ndani ya masaa 48.
Yanga ilifika kwenye mji huo juzi na imefanya mazoezi jana kujiandaa na mchezo huo ambao inahitaji ushindi au sare ili kuweza kutinga hatua ya makundi.
Ushindi wa mabao 2-0 iliyopata nyumbani April 07, ni mtaji mkubwa kwa Yanga kuelekea mchezo huo.

ADVERTISE HERE