Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewapongeza Wananchi wa Mbeya kwa kujitokeza kwa wingi kupokea Makombe yao katika shamrashamra zilizofanyika mkoani humo
Yanga inaendelea na kampeni ya kuandikisha Mashabiki na Wanachama wapya ambapo oparesheni hiyo inafanyika mkoa kwa mkoa
Mashabiki wa Yanga katika maeneo ambayo timu ya hamasa inapita, wanapata fursa ya kushuhudia makombe ambayo timu yao ilishinda msimu uliopita
Hersi amesema tukio ambalo limefanyika mkoani Mbeya leo ni la aina yake na anaamini hakuna timu imewahi kufanya tukio kama hilo barani Afrika
"Niwapongeze sana mlioratibu tukio la leo hapo Mbeya. Sidhani kama kuna timu Afrika ilishawahi kuandaa Tukio hili la Wanachama na kupata mapokezi makubwa aina hii"
"Mmenifurahisha sana kwa idadi kubwa ya watu waliolipia Uwanachama wao leo na mimi nina waahidi nitawafurahisha itakapofika SAA 6:00 USIKU," alisema Hersi