Usiku wa kuamkia leo Yanga ilitambulisha usajili wa mlinzi wa kushoto Chadrack Boka kutoka Fc Lupopo ya DR Congo
Katika usajili wa dirisha hili, Yanga imezingatia ubora wa mchezaji na uzoefu wake katika michuano ya Kimataifa
Boka amekuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo mara kadhaa ambapo ameichezea timu hiyo mechi sita za Kimataifa
Kabla ya kutua Fc Lupopo 2021, Boka aliwahi kuzitumikia Sanga Balende na TP Mazembe zote za DR Congo
Ndiye aliyekuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Lupopo mbele ya Valentin Nouma aliyesajiliwa na Simba
Boka alicheza zaidi ya asilimia 80 ya mech za msimu mzima akianza katika mechi zote 10 za michuano ya CAF
Yanga haikuachana na Lomalisa kwa sababu ya kushuka kiwango, bali ilizingatia umri na uhakika wa mchezaji kutumika katika mechi nyingi
Boka ana umri wa miaka 24 na hana historia ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake