Mijadala imekuwa mingo huko mitandaoni hasa baada ya kauli ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kuhusu mustakabali wa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki
Wengi wameingia 'ubaridi' baada ya kumsikia Injinia akisema kuwa bado Ki hajasaini mkataba na mazungumzo bado yanaendelea lakini akiwa na matumaini kuwa mfungaji huyo bora wa ligi kuu 2023/24 atabaki Jangwani
Taarifa zisizo na shaka kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa Aziz Ki yupo sana, na msimu ujao ataitumikia Yanga
Aidha mapema leo Yanga ilitangaza kumsajili Aziz mwingine (Andambwile) na kuwa msimu ujao kikosi cha Yanga kitakuwa na Aziz wawili
Andambwile ni miongoni mwa wachezaji mafundi kwelikweli katika ligi kuu ya NBC ndani ya misimu hii mitatu iliyopita
Huu ni wakati sahihi kwake kuitumika Yanga ambayo imesheheni mafundi wa boli hasa katika nafasi anayocheza ya kiungo mkabaji
Atakuwa na kazi ya kuchuana na Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Salum Abubakar 'Sure Boy' na Khalid Aucho 'The tank'