Leo Julai 11 2024 droo ya hatua ya awali na raundi ya kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL) na kombe la Shirikisho CAF CC itafanyika huko Misri
Kwa mujibu wa kalenda ya michuano hiyo, mechi za hatua ya awali mtoano zitaanza August 16-18 na marudiano ni August 23-25
Mechi za raundi ya kwanza zitapigwa Septemba wakati hatua ya makundi itaanza Oktoba 2024
Timu tano hazitashiriki hatua ya awali ambazo ni Al Ahly, Esperance, Mamelodi, Petro Atletico na TP Mazembe
Yanga iko katika kundi la timu nne ambazo zina alama za juu pamoja na CR Belouizdad, Raja CA na Pyramids
Katika hatua ya awali timu hizi zitapangwa dhidi ya timu ambazo haziko katka rank yoyote
ADVERTISE HERE