Usajili wa Duke Abuya unakwenda kuimarisha safu ya washambuliaji wa pembeni katika kikosi cha Kocha Miguel Gamondi
Yanga ilimtambulisha Abuya juzi na moja kwa moja akaungana na wenzake Avic Town katika maandalizi ya pre-season kuelekea msimu wa 2024/25
Usajli wake haukuwa na tetesi nyingi, lakini nyota huyo alisajiliwa kwa mapendekezo ya Gamondi mwenyewe
Kabla ya usajili wake, Yanga ilikuwa ikihusisha na mawinga kadhaa lakini Muargentina huyo akahitaji aletewe Abuya
Akizitumikia Singida Big Stars na Ihefu (sasa Fountain Gate na Singida Big Stars), msimu uliopita Abuya alihusika katika mabao nane akifunga manne na kutoa assist nne
Kabla ya kutua Singida, Duke aliitumikia Police FC Ligi Kuu ya Kenya ambapo alikuwa na msimu bora sana baada ya kumaliza msimu wa 2022-23 kwa kucheza mechi 31 ambazo alihusika kwenye jumla ya magoli 26 akifunga mabao 6 na kutoa assist 20
Aina yake ya uchezaji unaweza kumfananisha na Maxi Nzengeli kwani ni mchezaji 'mbishi' hasa anapokuwa na mpira mguuni
Tofauti yake na Maxi pengine ni kwa kuwa yeye hupendelea zaidi kucheza winga wakati Maxi ni kiraka anayependa kutumika katika eneo la kiungo