Msimu ujao Yanga itaendelea kubaki katika ulinzi wa mabeki wazawa Ibrahim Bacca, Bakari Nondo Mwamnyeto na Dickson Job
Ubora ulioonyeshwa mabeki hao msimu uliopita, unaipa Yanga matumaini ya kuendeleza pale walipoishia hasa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa
Ni sahihi kusema Bacca, Nondo na Job ni miongoni mwa mabeki bora katika ngazi ya klabu barani Afrika kwa sasa
Katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita na hata kombe la Shirikisho ambalo Yanga ilicheza fainali 2022/23, mabeki hao waliingia katika vikosi bora vya wiki vya CAF
Haijawa rahisi kwa mabeki wageni Mamadou Doumbia na Mganda Gift Fred kupenya mbele ya vitasa hao wazawa
Doumbia aliondoka baada ya miezi sita wakati Fred nae anaondoka baada ya msimu mmoja tu

ADVERTISE HERE