Shamara shamra za kuelekea wiki ya Mwananchi zinaanza mapema tu mwaka huu ambapo leo baadhi ya viongozi wa Yanga wataelekea Ikwiriri, Rufiji kwa ajili ya uzinduzi wa Shangwe kuelekea August 04 ambapo wiki ya Mwananchi itahitimishwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Msemaji wa Yanga Ali Kamwe amesema wiki ya Mwananchi mwaka huu itakuwa ya aina yake na ndio maana wameanza mapema 'amsha-amsha'
"Nimepokea meseji nyingi kutoka kwa mashabiki wa Yanga kutoka ndani na nje ya nchi, wakinitaka nitangaze viingilio mapema"
"Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Wananchi wana shauku kubwa ya kuishuhudia timu yao, kuwashuhudia wachezaji wapya kina Clatous Chama, Prince Dube, Aziz Ki na nyota wote tutakaowatambulisha kuiwakilisha Yanga msimu huu"
"Jumatatu (leo) tunaelekea Ikwiriri kuzindua shangwe la Wiki ya Mwananchi. Niwaambie tu, mwaka huu tumeandaa mambo mazuri, mashabiki wetu wakae tayari kwa tukio kubwa la kihistoria," alitamba Kamwe
Uzinduzi rasmi wa wiki ya Mwananchi unatarajiwa kufanyika Julai 27 ambapo Wananchi watashiriki matukio mbalimbali ya kijamii