Timu ya As Maniema Union ya DR Congo anatarajiwa kuwasili nchini baadae leo kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/25
Maniema wanatua nchini kwa hisani ya Yanga ambapo pre-season yao wataifanya katika viwanja vya Avic Town, yalipo Makao ya Yanga
Yanga inatarajiwa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya awamu ya pili ya program za pre-season ambapo mabingwa hao wa Tanzania Bara wanatarajiwa kushiriki michuano mbalimbali
Katika mahojiano aliyofanya na wanahabari akiwa Afrika Kusini hivi karibuni, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja wa klabu barani Afrika (ACA), alisema ujio wa Maniema ni sehemu ya mpango wa kukuza ushirikiano baina ya Yanga na klabu hiyo

ADVERTISE HERE