Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema bado mabingwa hao wa nchi hawajakamilisha usajili, kuna nyota wengine watawatambulisha
Baada ya kutangaza usajili wa Duke Abuya, ukimya umetawala Jangwani lakini baadhi ya wachezaji ambao hawajatambulishwa wanaonekana kushiriki mazoezi katika viunga vya Avic Town
Kamwe amesema kila mchezaji aliyesajiliwa na Yanga atatambulishwa na pia akiwahakikishia Wananchi juu ya ujio wa 'vyuma' zaidi
"Bado hatujamaliza, mashabiki wetu waendelee kufuatilia vyanzo vyetu vya habari kwani kila mchezaji ambaye tumemsajili atatambulishwa"
"Msimu huu tumeweka malengo makubwa, tunamshukuru Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa kuhakikisha kila mchezaji aliyehitajika katika hii project yetu anapatikana," alisema Kamwe
Mpaka sasa Yanga imetambulisha nyota sita wapya ambao ni mlinda lango Aboubakar Khomein, Chadrak Boka, Aziz Andambwile, Duke Abuya, Clatous Chama na Prince Dube
Mshambuliaji Jean Baleke tayari ameonekana mazoezini Avic Town licha ya kuwa bado hajatambulishwa rasmi
Aidha Yanga pia huenda ikaongeza beki mwingine wa kati mzawa kuchukua nafasi ya Gift Fred ambaye taarifa zinadai atatolewa kwa mkopo