Yanga imethibitisha kuwa wachezaji Khalid Aucho na Djigui Diarra wameungana na wenzao Avic Town katika pre-season inayoendelea
Nyota hao walirejea nchini jana baada ya kumaliza muda wa mapumziko ambayo wachezaji wote walipewa
Aidha ujio wa wachezaji hao unakamilisha idadi ya wachezaji wote ambao ni sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao
Ni pamoja na Kennedy Musonda ambaye nae alishawasili
"Kurejea kwa wachezaji hao kunafanya kikosi chetu hivi sasa kuwa kamili katika maandalizi kuelekea msimu ujao baada ya kambi kuanza wiki iliyopita Julai 08," sehemu ya taarifa ya Yanga ilibainisha
Aucho na Diarra wote waliongeza mikataba ya kuendelea kuitumikia Yanga mpaka mwaka 2026
Ni sehemu ya wachezaji muhimu katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi kuelekea 2024/25