VAR ni rasmi Ligi Kuu 2024/25

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jul 2024
VAR ni rasmi Ligi Kuu 2024/25

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo amezindua Teknolojia ya Usaidizi wa Mwamuzi kupitia Video (VAR) kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Vifaa hivyo ni vilivyotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) pamoja na Azam Media Limited

Teknlojia ya VAR inategemea kutumika kuanzia msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara 2024/25

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema teknolojia hiyo itasaidia kupunguza malalamiko yatokanayo na makosa ya waamuzi

"VAR itapunguza Manunguniko na makosa ya kibinadamu, sisi kama TFF tumeandika barua kuomba kibali cha kutumia VAR kwenye ligi yetu, " alisema Karia

Katika hatua nyingine, Karia amesema licha ya maoni ya wadau kuhusu kupunguza idadi ya wachezaji wa 12 wa kigeni, idadi hiyo itaendelea kutokana na faida ambazo ligi na klabu zinapata sababu ya ujio wa wachezaji hao

"Tumeamua kusisitiza kubaki na wachezaji wengi wakigeni licha ya watu wengi kutaka wachezaji wakigeni wapunguzwe"

"Mafanikio ambayo tumeyapata ni kwasababu ya uwepo wa wachezaji wakigeni ambao kabla ya wao kuja timu zetu zilikuwa hazifanyi vyema katika michuano ya kimataifa"

"Kwa takwimu tulizonazo wachezaji wakigeni hawajafika 70 kati ya wachezaji 600 ambao huwa wanashiriki katika ligi kuu,hivyo wachezaji wetu wanatakiwa na wao watoke nje ili wakapate changamoto na sio sisi kupunguza idadi ya wachezaji wakigeni,"alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’