Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Wolaitta Dicha Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City Jumapili ijayo April 22, 2018 yaani siku nne kuanzia leo.
Ikumbukwe Yanga iko nje ya nchi huko Ethiopia na pengine itainza safari ya kurejea jijini Dar es salaam kesho Alhamisi, zitakuwa zimebaki siku tatu kabla ya mchezo dhidi ya Mbeya City.
Upo uwezekano mkubwa Yanga ikawasili jijini Dar es salaam usiku hapo kesho hivyo sidhani kama wataweza kuunganisha moja kwa moja mkoani Mbeya.
Kwa vyovyote itakavyokuwa, kama mchezo huu hautasogezwa mbele japo kwa siku moja, Yanga itakuwa imekwenda Mbeya kukamilisha ratiba tu kwani itakuwa na siku moja tu ya kupumzika/kujiandaa na mchezo huo.
Hapa TFF walipaswa wawe waungwana kwa Yanga. Kushiriki kichuano ya Kimataifa kusiifanye Yanga 'iadhibiwe' kwa kuipangia ratiba isiyo rafiki ya michezo yake ya viporo.
Mazingira kama haya ndiyo yanafanya wengi wadhanie kuna namna inafanywa kurahisishia Simba kutwaa ubingwa.

ADVERTISE HERE