Kikosi cha Yanga kesho Alhamisi kinaelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano maalum ya pre-season ambayo Wananchi wamealikwa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kitashiriki michuano ya Mpumalanga Premier's International Cup ambapo Yanga itacheza mechi mbili
Mchezo wa kwanza ni Julai 20 dhidi ya Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), mchezo huo utahudhuriwa na mashabiki na kuonyeshwa mbashara na vituo vya televisheni
Mchezo wa pili utapigwa Julai 24 dhidi ya Ts Galaxy ya Afrika Kusini. Mchezo huo hautahudhuriwa na mashabiki wala kurushwa mbashara na vituo vya televisheni
Julai 28 Yanga itacheza mchezo wa tatu dhidi ya Kaizer Chiefs katika michuano ya Toyota Cup
Yanga itarejea Dar es salaam Julai 30 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi August 04