Duke Abuya na Aziz Andambwile walipotambulishwa kusajiliwa na Yanga hakukuwa na mijadala mingi mitandaoni pengine ni kwa kuwa wengi waliamini ni wachezaji wa kwenda kuongeza idadi tu pale kwa Wananchi
Lakini dakika 45 walizocheza jana kwenye mchezo dhidi ya Augsburg zimedhihirisha kwa nini Kocha Miguel Gamondi aliwahitaji
Kuingia kwao kuliimarisha eneo la kiungo na kuifanya Yanga ikae na mpira na kupeleka mashambulizi mengi langoni kwa Augsurg
Kasi ya Abuya ilikuwa tatizo kwa walinzi wa Augsburg. Licha ya Wajerumani hao kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, Yanga iliwapa mechi nzuri sana katika kipindi cha pili
Haitashangaza kuona Abuya na Andambwile wakachukua nafasi katika kikosi cha kwanza kwani mapema tu wamemkosha Gamondi
ADVERTISE HERE