Gamondi afurahia ushindani kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2024
Gamondi afurahia ushindani kikosi cha kwanza

Katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi msimu huu ni wazi haitakuwa rahisi kwa wachezaji kujihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza

Ushindani umeanza mapema dalili zinaonekana kwani kila mchezaji anayepata nafasi ya kucheza katika mechi hizi za pre-season anajituma kwelikweli

Gamondi amesema ushindani huo ndio aliohitaji kwani utamfanya kuwa na timu yenye wachezaji wanaojituma sana uwanjani

"Ushindani wa namba umeongeza kitu kikubwa kwa wachezaji na kuwafanya wawe na ari ya kupambana, kwani hakuna anaejiamini atapata nafasi kutokana na ubora wa kila mmoja wapo"

"Ninafurahia jambo hilo kwani limewafanya wachezaji kujituma na kutafuta nafasi na hizo ni sifa za mchezaji anayecheza kwa malengo"

"Kikosi tulichosajili ni kwa malengo yetu ya msimu ujao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na ya ndani, hatukuhitaji kuruhusu wachezaji wetu bora waondoke, nafahamu zimekuja ofa nyingi lakini napongeza uongozi,  tumeweza kulinda mipango yetu ya msimu ujao," alisema

Jana Yanga ilicheza mechi ya pili ya Mpumalanga Premier's International Cup dhidi ya TS Galaxy ambayo ilimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Katika kipindi cha kwanza Gamondi alitumia nyota wote wazawa na wakamaliza kipindi hicho pasipo kuruhusu bao 

Alipofanya mabadiliko katika kipindi cha pili, Yanga iliongeza kasi zaidi na kufunga bao pekee kupitia kwa Prince Dube aliyemalizia pasi ya Stephane Aziz Ki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’