George Lwandamina 'Chicken Man'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2018
George Lwandamina 'Chicken Man'
Mafanikio iliyopata Yanga kutinga hatua ya makundi ya michuano ya CAF, kombe la Shirikisho yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na falsafa ya kocha George Lwandamina.

Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Dicha, baada ya presha ya dakika 20 za kipindi cha kwanza, wachezaji walituliza mchezo na kucheza kwa tahadhari kubwa.

Aidha mfumo wa kujilinda na kushambulia kwa kushitukiza umekuwa ukiinufaisha sana Yanga katika michezo yake mingi.

Wapo wanaokosoa kwamba Yanga ya sasa haichezi 'sexy football' kama ilivyokuwa enzi za Pluijm lakini jambo moja la uhakika ni kuwa Yanga ya sasa ni makini zaidi kuliko ile ya Pluijm.

Tunaweza kusema Yanga ya sasa haifungwi 'kizembezembe' kama zamani. Takwimu zinadhihirisha hilo.

Yanga ingekuwa na Lwandamina hatua hii ya makundi, ingefanya miujiza zaidi.

Hakuna aliyetegemea kama Yanga itafika hapo ilipo, lakini ni kocha Lwandamina aliyejenga saikolojia ya wachezaji na kuwafanya wajiamini.

Winga Yusuph Mhilu aliwahi kulizungumza hilo, kuwa Lwandamina aliwaweka chini na kuwapa somo kuwa wao ndio wanategemewa, hasa kipindi ambacho kulikuwa na majeruhi wengi.

Haikuwa kazi rahisi kufanikiwa kuwaondoa Wolaitta Dicha kwenye ardhi yao. Kama si umakini wa kujilinda na umahiri wa mlinda lango Youthe Rostand, mambo yangekuwa tofauti.

Hawa Dicha waliwachapa Zamaleki kwenye dimba lao mabao 2-1 na kufanikiwa kuwatoa kwa matuta kwenye mchezo wa marudiano nchini Misri baada ya kuchapwa mabao 2-1.

Ushindi dhidi ya Zamalek ulidhihirisha kuwa hii haikuwa timu ya mchezo mchezo. Hata aina yao ya uchezaji inaonyesha.

Lakini ushindi wa mabao 2-0 iliyopata Yanga nyumbani umekuwa mtaji wa faida, na sasa imesonga mbele hatua inayofuata.

Yanga inatarajiwa kucheza michezo sita katika hatua ya makundi, mitatu nyumbani na mitatu ugenini.

Kwa kikosi hiki, Yanga inaweza kumaliza nafasi mbili za juu na kutinga hatua ya robo fainali.

Hakika mchango wa Lwandamina aliyejenga kikosi imara unapaswa kuheshimiwa, kama yalivyo maamuzi yake ya kuondoka kwa hiari.

Imekuwa bahati mbaya alishindwa kuvumilia zaidi changamoto zilizokuwa zinaikabili klabu. Maamuzi yake yaheshimiwe kwani naye ni binadamu.

Naamini huko aliko anatamani kurejea ili amalizie kazi kubwa aliyoianza.

Naamini baada ya mafanikio haya, Yanga mpya yenye uwezo wa kichumi inakwenda kuzaliwa.

Ukifanyika uwekezaji wa kutosha, Yanga inaweza kuwa moja ya vigogo wa soka Barani Afrika. Imekuwa ikiimarika Kimataifa mwaka hadi mwaka

May 05 Mkutano Mkuu wa wanachama utafanyika, moja ya ajenda bila shaka itakuwa kupitisha mapendekezo ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’