Kiungo Mudathir Yahya ameendeleza pale alipoishia msimu uliopita juzi akiifungia Yanga bao la kusawazisha katika mchezo dhidi ya Red Arrows
Ulikuwa mchezo wa kuhitimisha shamra shamra za wiki ya Mwananchi uwanja wa Benjamin Mkapa Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Zambia ambao pia ni mabingwa wa CECAFA Kagame Cup
Bao la pili lilifungwa Stephane Aziz Ki katika dakika za jiooooni kwa mkwaju wa penati kufuatia Nickson Kibabage kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari
Mudathir alionyesha kiwango bora katika mchezo huo na pengine angeweza kufunga mabao zaidi kama sio uimara wa mlinda lango wa Red Arrows Charles Kalumba
Ujio wa Duke Abuya kikosini ni kama umeongeza ushindani katika eneo la Mudathir lakini ni wazi bado Muda anaweza kuendelea kuaminiwa na kocha Miguel Gamondi kwa sababu ya uwezo wake wa kufunga mabao