Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) Almas Kasongo amesema wiki hii watatangazi rasmi ratiba ya Ligi Kuu Bara 2024/25
Sambamba na kutangaza ratiba, TPLB pia itatangaza maboresho ya kanuni za ligi zitakazotumika 2024/25
Kasongo amesema wamechukua muda kuiandaa ratiba hiyo na anaamini haitakuwa na changamoto na mabadiliko ya mara kwa mara
"Ratiba ya ligi pamoja na maboresho ya kanuni zipo tayari na ndani ya siku hizi mbili ofisa habari wa ligi ataweka hadharani"
"Ni kweli tulikuwa kimya kwa muda mrefu, lakini kimya kirefu kina mshindo, hivyo tunaamini ratiba ya msimu huu itakuwa bora," alisema Kasongo
Msimu wa Ligi Kuu Bara 2024/25 unatarajiwa kuanza rasmi Agosti 16, Yanga wakiwa mabingwa watetezi wakishikilia taji kwa misimu mitatu mfululizo