Ramadhani Kabwili(17), kipa namba moja wa Serengeti Boys leo amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia Yanga, mabingwa wa kihistoria wa soka la Tanzania.
Kabwili amesaini mkataba huo leo baada ya kurejea kutoka Rwanda alikokuwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
Kinda huyo amekamilisha idadi ya makipa watatu wa kikosi cha kwanza cha Yanga.
Makipa wengine ni Youthe Rostand na Kakolanya.
Yanga imeachana rasmi na magolikipa wake wawili ambao ni Deo Munishi 'Dida' aliyetimkia klabu ya University of Pretoria ya Afrika Kusini na Ali Mustafa 'Barthez' aliyesajiliwa na Singida United.

ADVERTISE HERE