Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 09,2024 imetupilia mbali mwenendo mzima wa maombi yaliyofunguliwa na Juma Magoma na wenzake ya kutaka kuundoa uongozi wa klabu ya Yanga madarakani na pia kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa, katika hukumu iliyowapa ushindi Wazee hao
Mahakama hiyo imeamuru Magoma, Geofrey Mwaipopo na Abeid Mohamed Abeid walipe kwa Muombaji ( Bodi ya Wadhamini ya klabu ya Yanga) gharama za uendeshaji wa shauri hilo
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, wakati akitoa uamuzi wa marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022 yaliyoombwa na Bodi hiyo kwa madai kuwa Wazee hao hawakuwa na sifa ya kufungua shauri
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amesema gharama za uendeshaji wa kesi hiyo ni zaidi ya Milioni 70, Magoma na wenzake watalazimika kulipa gharama hizo