Kiungo Yusuf Kagoma ameingia matatani baada ya Yanga kuwekea pingamizi usajili wake na Simba
Juzi Kagoma alikwama kuitumikia Simba katika mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii kutokana na pingamizi hilo
Yanga imethibitisha kumsajili Kagoma ambapo alilipwa sehemu ya fedha za usajili wake lakini akasaini mkataba na klabu ya Simba
Kabla ya kumalizana na mchezaji, Yanga ilianza kwa kumalizana na Singida FG ambayo alikuwa bado na mkataba wa mwaka mmoja
Singida FG wamethibitisha walifanya biashara na Yanga na sio klabu ya Simba
Yanga haimuhitaji Kagoma tena lakini imefungua madai hayo ikitaka ilipwe fedha ilizotumia katika mchakato wote
ADVERTISE HERE