Timu ya Vital'o kutoka Burundi iko nchini tangu wiki iliyopita ikijiandaa na mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumamosi, August 17 katika uwanja wa Azam Complex
Jumamosi iliyopita timu hiyo ilikuwa Mwanza ambapo ilichuana na Pamba katika Pamba Day katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba na kumalizika kwa sare ya bao 1-1
Baada ya mchezo huo Vital'o walielekea Dar es salaam ambapo timu hiyo inafanya mazoezi katika uwanja wa KMC
Katika hatua nyingine, kikosi cha Yanga leo kinarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya kuikabili Vital'o siku ya Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex
Juzi Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Azam Fc mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Wananchi watakuwa na siku nne za kukamilisha maandalizi kabla ya mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali
Mechi ya mkondo wa pili katika hatua hiyo itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, August 24
Yanga imepata ahueni ya kucheza mechi zote Tanzania baada ya Vital'o kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya CAF katika nchi yao