Hatutawadharau Vital'o - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2024
Hatutawadharau Vital'o - Gamondi

Kuelekea kwenye mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hatowadharau wapinzani wao Vital'o ya Burundi licha ya michezo yote kufanyika hapa nchini

Gamondi, alisema anafahamu umuhimu na faida ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani, lakini watamuheshimu mpinzani wao kwa kuwa soka ni mchezo wenye matokeo ya kushangaza wakati mwingine

Vital'o walichagua uwanja wa Azam Complex kuwa uwanja wao wa nyumbani baada ya CAF kuwagomea kucheza Burundi baada ya kukosa uwanja unaokidhi vigezo

Gamondi amesema anakiandaa kikosi chake kikamilifu ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo na kusonga mbele hatua inayofuata

"Tunajiandaa kikamilifu, mchezo hautakuwa mwepesi kama inavyodhaniwa, najua wapinzani wetu licha ya kucheza hapa Tanzania michezo yote, wamejiandaa vizuri, tutakabiliana nao kwa tahadhari," alisema Gamondi

Yanga wanatarajia kuumana na Vital'o, Agosti 17 kwenye mchezo wa kwanza ambao Warundi hao watakuwa wenyeji kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kabla ya kurudiana wiki moja baadaye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao Yanga watakuwa wenyeji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’