Meneja Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji wote waliosajiliwa na mabingwa hao wa nchi wana nafasi sawa ya kucheza kwa kuzingatia matakwa ya benchi la ufundi
Kamwe amekanusha taarifa za uzushi zilizosambazwa mitandaoni zikidai mkataba wa kiungo Clatous Chama una kipengele cha kumuhakikishia kucheza katika kikosi cha kwanza katika kila mechi
Kamwe amesema wachezaji wote wana nafasi sawa ya kucheza mbele ya Kocha Miguel Gamondi kwa kuzingatia mahitaji ya mechi husika kwani Yanga imesajili wachezaji 27 huku wakitakiwa kuanza wachezaji 11 tu katika kila mechi
"Ifahamike wachezaji wote wana nafasi sawa katika kikosi cha Yanga. Hakuna kipengele kinachotaka Clatous Chama aanze katika kikosi cha Yanga kwenye kila mechi
"Na sio Chama tu mchezaji yoyote wa Yanga, hakuna kipengele kinachotaka aanze kikosi cha kwanza"
"Hizi ni propaganda za watu wameanzisha kwa sababu wanatafuta faraja," Kamwe aliiambia UFM
Tangu Chama aliposajiliwa na Yanga, zimeibuliwa propaganda za kila aina ili tu kujaribu kumchonganisha mchezaji na klabu pamoja na mashabiki