Licha ya kuwasili usiku wa manane, idadi kubwa ya mashabiki wamejitokeza uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuipokea Yanga iliyotoka nchini Ethiopia.
Yanga imewasili usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba ikitoka Addis Ababa, Nairobi na kisha Tanzania.
Yanga imefanikiwa kufuzu hatua ya Makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kuichapa Wolaiita Dicha kwa jumla ya mabao 2-1 (2-0, 0-1).
Droo ya hatua hiyo inatarajiwa kufanyika jiji la Cairo, nchini Misrti kesho.
Baada ya kurejea jijini, Yanga inatarajiwa kuunganisha mkoani Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City itakaopigwa keshokutwa Jumapili, April 22 kwenye dimba la Sokoine

ADVERTISE HERE