Yanga haikukurupuka kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' ambaye aliitumikia Simba kwa misimu mitano kabla ya kutua kwa Wananchi msimu huu
Uzoefu wake hasa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ni moja ya sababu iliyomfanya Rais wa Injinia Hersi Said kuhakikisha fundi huyo wa mpira anatua Yanga
Chama hakuhitaji muda mrefu kudhihirisha thamani yake katika michuano ya Kimataifa jana akifunga moja ya mabao katika ushindi wa 4-0 ambao Yanga walipata dhidi ya Vital'o katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ya ligi ya mabingwa
Ulikuwa mchezo wa 56 kwa Chama katika michuano hiyo ambapo bao hilo alilofunga lilikuwa la 19 huku pia akiwa na assist 8
Katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote katika michuano ya ligi ya mabingwa, Chama anashika nafasi ya 6