Yanga inaweza kukutana na CBE Ethiopia hatua inayofuata CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Aug 2024
Yanga inaweza kukutana na CBE Ethiopia hatua inayofuata CAF CL

Kuna uwezekano mkubwa Yanga itachuana na CBE ya Ethiopia katika mchezo wa kusaka tiketi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kama timu hiyo italinda ushindi wa ugenini iliyopata dhidi ya SC Villa ya Uganda katika mchezo wa mkondo wa kwanza

CBE ndio mabingwa wa ligi kuu ya Ethiopia wakitwaa ubingwa huo msimu uliopita ikiwa ni mara yao ya kwanza na kukata tiketi ya michuano ya ligi ya mabingwa. Waliichapa SC Villa mabao 2-1 nchini Uganda

Aidha kwa upande wa Yanga, baada ya ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex Jumamosi iliyopita, Kocha Miguel Gamondi aliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku moja

Akizungumza baada ya mchezo huo, Gamondi alisema licha ya ushindi huo mnono, bado kikosi chake hakijafuzu hatua inayofuata hadi pale watakapowatoa Vital'o

"Bado hatujafuzu, hizi ni dakika 90 za kwanza nani anajua kipi kitatokea katika mchezo wa marudiano, tutapumzika kwa siku moja baada ya hapo tutarudi kujipanga kwa mechi hiyo," alisema Gamondi

Katika mchezo wa marudiano Yanga inahitaji ushindi au sare tu ili kusonga mbele hatua inayofuata na kama SC Villa watashindwa kupindua matokeo ugenini wakihitaji kushinda kuanzia mabao 2-0,  wataipa nafasi Commercial Bank ya Ethiopia kusonga mbele na kuchuana na Yanga

Habari njema kwa Yanga ni kuwa changamoto ambazo CBE wamekutana nazo hazina tofauti na changamoto walizokutana nazo Vital'o, kwani timu hizo hazichezi mechi zao za nyumbani katika nchi zao kwa kuwa hawana viwanja vinavyokidhi vigezo vya CAF

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’