Kikosi cha Yanga baadae leo kinatarajiwa kuelekea mkoani Kagera tayari kwa mechi ya kwanza ya ligi kuu msimu huu, 2024/25
Mabingwa hao watetezi kwa misimu mitatu mfululizo, wanaanza kampeni ya msimu mpya kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Alhamisi, August 29 katika uwanja wa Kaitaba
Ni msimu mwingine wa kusaka makombe kwa Yanga kwani kikosi cha kocha Miguel Gamondi bado kina njaa kali ya mataji
Pengine msimu huu vilio vitakuwa vingi zaidi kwa wapinzani! kikosi cha Yanga kimekuwa bora zaidi kuliko kilivyokuwa msimu uliopita
Yanga inakwenda Kagera ikiwa na kumbukumbu ya kukosa alama zote tatu katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa uwanja wa Kaitaba msimu uliopita ambao ulimalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
KMC ilikuwa timu ya kwanza kuonja vipigo vya Yanga msimu uliopita ambapo ilipigwa mabao 5-0 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa dimba la Azam Complex
Kabla hata ya ligi kuanza, Yanga tayari imetembeza vipigo vikubwa msimu huu kwa timu kama Kaizer Chiefs (4-0), Azam Fc (4-1), Vital'0 (4-0 na 6-0) katika ligi ya mabingwa
Je Kagera Sugar wataweza kuzuia mafuriko haya ya Wananchi...?