Kiungo wa Yanga Duke Abuya amejumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu Afcon 2025 dhidi ya Namibia na Zimbabwe
Abuya ni miongoni mwa nyota wapya waliosajiliwa na Yanga katika dirisha lililopita la usajili
Mwanzo wake bora na Yanga imekuwa chachu kwake kujumuishwa katika kikosi cha Harambee Stars
Takribani nyota 9 wa Yanga wamejumuishwa katika vikosi vya timu za Taifa na wengine zaidi wanatarajiwa kuitwa
Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Dickon Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya, Clement Mzize, Abuya na Prince Dube tayari wamepokea wito kutoka timu zao za Taifa huku
Nyota wengine wa kigeni ambao wanatarajiwa kujiunga na timu za Taifa ni Djigui Diarra (Mali), Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), Kennedy Musonda na Clatous Chama (Zambia)