Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema anatarajia msimu huu utakuwa na ushindani zaidi lakini ana matumaini makubwa ya kikosi chake kufanya vizuri
Yanga inaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo kwa kuumana na Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba, Alhamisi August 29
"Tuko tayari kwa msimu mwingine wa ligi, natarajia msimu huu utakuwa mgumu zaidi kuliko uliopita kwani naamini kila timu inajianda kwa ajili ya kupambana nasi"
"Lakini nina imani zaidi na timu yangu kuliko msimu uliopita. Sasa nawafahamu vyema wachezaji wangu wote baada ya kufanya nao kazi kwa mwaka mzima"
"Tumeongeza wachezaji saba wapya ambao naamini pia wataongeza nguvu zaidi katika timu yetu"
"Tumekuwa na wakati mzuri wa maandalizi na jambo la muhimu tunakwenda kushindana tukiwa na lengo la kutwaa ubingwa kwa mara nyingine ingawa natambua wakati huu haitakuwa rahisi pia," alisema Gamondi
Tangu alipojiunga na Yanga msimu uliopita, Gamondi ameiongoza Yanga kutwaa mataji matatu, Ligi Kuu, FA na Ngao ya Jamii
Aidha msimu uliopita Gamondi aliingoza Yanga kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kusubiri kwa miaka 25
Yanga imeweka malengo makubwa zaidi msimu huu kushinda mataji yote ya ndani pamoja na kufanya vizuri zaidi katika ligi ya mabingwa