Msimu uliopita mlinzi wa kati Dickson Job ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao kwa Yanga katika ligi kuu ya NBC 2023/24 mchezo dhidi ya KMC uliopigwa uwanja wa Azam Complex na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-0
Leo tena Wananchi wanakwenda kutafuta rekodi nyingine dimba la Kaitaba, Yanga ikitarajiwa kuchuana na Kagera Sugar katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu kwa Yanga msimu huu 2024/25
Wenyewe Wananchi wanasema ligi haiwi imeanza mpaka pale Yanga inapocheza hivyo unaweza kusema pazia la ligi kuu ya NBC linakwenda kufunguliwa rasmi leo na Wananchi
Je ni nani atafunga bao la kwanza la Yanga kwenye ligi msimu huu?
Jibu la swali hili litapatikana kuanzia saa 11 jioni pale dimba la Kaitaba wakati Yanga itakapokuwa mgeni wa Kagera Sugar
ADVERTISE HERE