Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameweka mkakati wa kuhakikisha kikosi chake kinapata ushindi nchini Ethiopia katika mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA ambao utapigwa Septemba 13 katika uwanja wa Abebe Bikila
Licha ya changamoto ya maandalizi ya mchezo huo akikosa nusu ya kikosi chake, wachezaji wakienda katika majukumu ya timu za Taifa, Gamondi amesema watakwenda Ethiopia wakiwa lengo moja tu, kushinda
"Tuna malengo kama timu ya kusonga mbele hatua ya makundi hivyo tunapaswa kupata matokeo mazuri ugenini na kuja kumaliza kazi hapa nyumbani"
"Hatuwafahamu vyema wapinzani wetu lakini jambo muhimu ni sisi kujiandaa upande wetu, kumjua mpinzani ni sehemu ndogo tu katika maandalizi"
"Tuna wachezaji 14 wameitwa timu zao za taifa hivyo hawatakua sehemu ya maandalizi yetu lakini tutaungana nao siku mbili hadi tatu kabla ya mechi, " alisema Gamondi
CBA iliiondosha SC Villa ya Uganda kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 ambapo Wahabeshi hao walipata ushindi wa mabao 2-1 ugenini na kulazimishwa sare ya bao 1-1 nyumbani
Yanga itasafiri kwenda Ethiopia kwa mechi ya mkondo wa kwanza itakayopigwa Septemba 13-15 na mchezo wa marudiano kupigwa Tanzania Septemba 20-22
Huenda mchezo huo ukapigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar