Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa Yanga inalihudumia soka la Afrika baada ya kutoa wachezaji 14 katika timu za Taifa
Kamwe amesema Yanga ndio klabu iliyotoa wachezaji wengi zaidi kwa timu za Taifa katika kipindi hiki na pengine hiyo inaweza kuwa ni rekodi ya kipekee
"Tumetoa wachezaji 14 katika timu za Taifa, hii ni rekodi katika kumbukumbu zangu haipo timu ambayo imetoa idadi kubwa wachezaji katik timu za Taifa kwa wakati mmoja kama ilivyofanya Yanga"
"Tumetoa wachezaji kwa mataifa nane barani Afrika hivyo ni sahihi kusema tunalihudumia soka la Afrika vizuri"
"Na hapa ndipo umuhimu wa kikosi kipana unapokuja. Licha ya wachezaji hao kukosekana, waliobaki wanaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya pili ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA"
"Tutakuwa na mechi moja ya kirafiki ambayo ni ya ndani, itafanyika katika uwanja wetu pale Avic Town. Wachezaji waliobaki wataungana na wenzao siku mbili au tatu kabla ya kusafiri Ethiopia kusaka matokeo muhimu ya kutupeleka hatua ya makundi ligi ya mabingwa," alisema Kamwe
Yanga itachuana na CBE SA kati ya Septemba 13-15 mchezo wa kwanza ukipigwa uwanja wa Abebe Bikila huko Ethiopia