Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mechi za Ngao ya Jamii kwa upande wa Wanawake zitapigwa Septemba 24-27 katika uwanja wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam
Simba Queens, JKT Queens, Yanga Princess na Ceasiaa zitachuana katika michuano hiyo inayoashiria ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake
Kwa mara nyingine, itashuhudiwa mechi ya dabi ambapo Simba Queens waliotwaa ubingwa msimu uliopita watachuana na Yanga Princess wakati JkT Queens wakiumana na Ceasiaa Queens katika mechi za nusu fainali
Simba na Yanga zilikutana pia kwenye nusu fainali kwa upande wa wanaume Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga fainali ambapo walifanikiwa kutwaa taji kwa kuifumua Azam Fc mabao 4-1
ADVERTISE HERE