Kuna rekodi ya aina yake kikosi cha Yanga kimeweka baada ya kushinda mechi 10 mfululizo ikiwa ni mechi za mashindano na mechi za kirafiki
Mara ya mwisho Yanga ilipopoteza mechi dhidi ya Augsburg katika michuano ya pre-season ya Mpumalanga Premiers International Cup
Katika mechi hizo, Wananchi wamepachika jumla ya mabao 29 huku wakiruhusu mabao mawili tu kutikisa nyavu zao
Unaweza kusema vijana wa Kocha Miguel Gamondi wameanza msimu na 'gia kubwa' ikiwa ni dalili njema ya msimu mwingine wa mafanikio
Licha ya mafanikio ya kushinda mataji kwa misimu mitatu mfululizo, bado wachezaji wa Yanga wana ari na morali kubwa ya kupambana
Aidha usajili uliofanyika katika dirisha lililopita umeongeza chachu ya ushindani miongoni mwa wachezaji kikosini
ADVERTISE HERE