Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amechangia matibabu ya kiungo wa zamani wa Polisi Tanzania Gerrard Mdamu ambaye alivunjika miguu katika ajali ya basi
Mdamu alihitaji Tsh 1.5M ili kukamilisha awamu ya pili ya matibabu yake ambapo Arafat ametoa kiasi hicho cha fedha
Taarifa iliyotolewa na Daktari bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi), Kennedy Nchimbi, alisema Mdamu anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu wake wa kulia
Daktari huyo alisema wakati wanamfanyia upasuaji wa kumtibu mguu wake wa kushoto, lengo la kwanza ilikuwa ni kuhakikisha anabakia na mguu wake, hilo lilifanikiwa
Sasa anahitaji kutengenezewa kiatu cha mguu wa kushoto, ambacho kitakuwa kinaakisi jinsi mguu ulivyopinda ambacho kitafidia mwanya wa juu, hivyo atakuwa na uwezo wa kutembea kukanyaga moja kwa moja
Wadau wameombwa kuendelea kumchangia Mdamu ambaye Julai 9, mwaka 2021 alivunjika miguu baada ya basi la timu ya Polisi Tanzania, kupata ajali wakitoka katika mazoezi Uwanja wa TPC kuelekea kambini