Kalenda ya mechi za kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2025 kwa timu za Taifa inatarajiwa kuhitimishwa kesho Jumanne katika viwanja mbalimbali
Nyota wa Yanga ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa watakuwa na muda mfupi wa kusafiri kujiunga na wenzao tayari kwa mechi za raundi ya pili ligi ya mabinggwa barani Afrika
Septemba 14 Yanga inapaswa kuwa Ethiopia kumenyana na CBE SA katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi CAF CL
Habari njema kwa Yanga ni kuwa kiungo Khalid Aucho ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Uganda atamaliza majukumu yake leo kwa mchezo dhidi ya Congo ambao utapigwa huko Uganda
Aucho huenda akajiunga na kikosi cha Yanga hapo kesho kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya safari ya kuelekea Ethiopia
Baadhi ya wachezaji wanaweza wakasafiri moja kwa moja Ethiopia kuungana na kikosi ili kuepuka uchovu wa kuunganisha safari
Nyota saba ambao wako na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wao watashuka dimbani kesho Septemba 10 huku Benin, mchezo ukitarajiwa kupigwa saa 1 usiku. Ni wazi itakuwa rahisi kwao kusafiri moja kwa moja Ethiopia
Zambia pia itachuana na Sierra Lione katika mchezo mwingine utakaowahusisha Kennedy Musonda na Clatous Chama ambao wanaweza kulazimika kuondoka baada ya mchezo huo ili kuungana na wenzao Dar tayari kuelekea Ethiopia
Zimbabwe ya Prince Dube itakuwa nyumbani kuchuana na Cameroon mechi itakayopigwa saa 1 usiku, wakati Kenya ya Duke Abuya ikiwa ugenini Namibia kuchuana na wenyeji wao
Djigui Diarra na Mali watakuwa ugenini Eswatini wakati Stephane Aziz Ki na Burkina Faso watakuwa nyumbani kuchuana na Malawi katika mechi itakayopigwa saa nne usiku
Ratiba ya mechi dhidi ya CBE SA imekaa 'kimtego' kwani mechi imepangwa kupigwa Jumamosi saa 9 Alasiri