Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imewatoa 'kimasomaso' Watanzania ugenini huko Ivory Coast ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2025
Stars ilitokea nyuma kupata ushindi huo muhimu kwa mabao ya Feisal Salum na Mudathir Yahya wakitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya Guinea
Ni ushindi unaoihakikishia Stars kushika nafasi ya pili baada ya kufikisha alama nne kundi H nyuma ya DR Congo iliyokusanya alama sita
ADVERTISE HERE