Gamondi kunoa makali safu ya ushambuliaji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2024
Gamondi kunoa makali safu ya ushambuliaji

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema kazi aliyokuwa nayo kuelekea mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE ya Ethiopia, ni kuhakikisha wanafanyia kazi eneo la umaliziaji

Akizungumza jijini Dar es Salaam, kocha huyo alisema kuelekea mchezo ujao atalifanyia kazi tatizo hilo ili lisijirudie tena kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

Gamondi alitoa sababu ambazo anaamini huenda zilisababisha hilo, lakini hataki liendelee kwa vijana wake

"Nahitaji kukaa nao na kuwaweka kwenye mtazamo na umakini ule ambao tumeuzoea, hii ya kukosa mabao nadhani imetokana na kutokuwa fiti pamoja na umakini"

"Sikuwa na wachezaji 14 ambao walikuwa kwenye vikosi vya timu za taifa, kitu ambacho kimesababisha wengi wasiwe kwenye viwango vya kawaida na umakini na hii huwa linatokea sana wachezaji wanapokwenda kwenye timu za taifa," alisema

Gamondi alibainisha kuwa katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, Ethiopia, walikosa jumla ya mabao saba ambayo kama wangeshinda wangekuwa wameimaliza mechi ugenini

"Sijafurahishwa na kiwango kwa sababu tumepoteza nafasi nyingi sana, tulikuwa tuimalize mechi kule kule kama tungepata nafasi zile kwa hiyo, ni lazima nilifanyie kazi kabla ya kukutana kwenye mechi ya marudiano"

Akizungumzia mchezo wa marudiano, alisema hautokuwa rahisi kama ambavyo wengi wanavyodhani, lakini akawataka mashabiki wa Yanga kufurika uwanjani kwani amewaandalia mambo mazuri

Katika mchezo wa Jumamosi Yanga ilishinda bao 1-0, lililofungwa na straika raia wa Zimbabwe, Prince Dube

Yanga inahitaji ushindi au sare yoyote ili kuweza kutinga hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo, ambapo msimu uliopita ilifanya hivyo na kuishia hatua ya robo fainali

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’