Wapinzani wa Yanga katika mchezo wa ligi ya mabingwa, CBE;Β wamewasili visiwani Zanzibar tayari kwa mtanange huo utakaopigwa Jumamosi, Septemba 21, saa 2:30 usiku
CBE SA watakuwa wageni wa Yanga katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex
Baada ya kutua uwanja wa ndege wa Zanzibar, maafisa wa timu hiyo walitamba kuwa wamekuja kupindua meza mbele ya mabingwa wa nchi na kufuzu hatua ya makundi
Kwa upande wa wenyeji Yanga, watatua visiwani Zanzibar kesho Alhamisi, timu ikitarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam na boti ya saa 3 asubuhi
Dimba la Amaan liko tayari kwa mtanange huo ambao utaamua timu itakayocheza hatua ya makundi kati ya Yanga au CBE
Yanga tayari iko mbele kwa bao 1-0 ukiwa ni ushindi waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ethiopia
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa wanahitaji kutinga hatua ya makundi kwa msimu wa pili mfululizo, hivyo wanafanya maandalizi kabambe kuhakikisha wanaibuka na ushindi Jumamosi