Arafat awaalika mashabiki New Amaan Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2024
Arafat awaalika mashabiki New Amaan Complex

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewataka mashabiki wa timu hiyo visiwani Zanzibar kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari mapema leo, Arafat alisema Yanga imedhamiria kuweka rekodi kwa kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wakiwa kwenye ardhi ya Zanzibar

"Klabu yetu kwa sasa ina lengo moja ya kuvunja rekodi ambazo hapo awali ziliwekwa au tumeshindwa kuzivunja. Ni heshima kubwa sana kwa Zanzibar kupata fursa ya kuvunja baadhi ya rekodi hizi. Yanga itaweka rekodi ya kutinga hatua ya makundi ikiwa Zanzibar tena kwenye uwanja mpya wa Amaan"

"Wanayanga wa Zanzibar tumejipanga kwa namna ya kipekee. Tumehakikisha Miundo mbinu yote ya kuipokea timu ipo sawa. Ni wajibu wetu sasa mashabiki kuhakikisha tunanunua tiketi kwa wingi. Huenda hizi tiketi kesho zikawa zimeisha. Natamani kuona uwanja wetu wa Aman ufurike"

"Nafahamu kuna watu wamejificha kwenye kichaka cha alama za CAF. Ni matarajio yetu tukishinda mchezo ujao tunakwenda kufyeka hicho kichaka cha alama. Hivyo nawasihi sana Mashabiki wafike kwa wingi tufyeke kichaka. Waliopo nje ya Zanzibar nao wafike, Zanzibar ni Njema yeyote aje," alisema Arafat

Nae Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewashukuru wadhamini waliojitokeza kudhamini mchezo kati ya Yanga dhidi ya CBE ambapo amebainisha kuwa klabu imeingiza zaidi ya Tsh Milioni 200 kutokana na udhamini

Kamwe amesema Jumamosi ni siku maalum kwa Yanga kufyeka kichaka cha wale waliokuwa wakitambia ubora katika mashindano ya CAF

"Nichukue fursa hii kuwashukuru sana Wadhamini ambao wamejitokeza kufanya kazi na sisi. Kuelekea mechi yetu dhidi ya CBE tayari tumeshakusanya zaidi ya Milion 200 nje ya mauzo ya tiketi"

"Asanteni sana wadhamini wetu. Jumamosi ni siku ya kwenda kufyeka kichaka cha kujifanya wao ni bora kuliko sisi kwneye rank za CAF. Haiwezekani timu tumeifunga goli 7 inakaa juu yetu sisi kwenye rank za CAF. Kila Mwanayanga anapaswa kuhakikisha hii ni jumamosi ya kuhakikisha tunakwenda kukaa juu"

"Leo na kesho Kikosi kitafanya mazoezi jioni hapa Zanzibar. Kesho (ijumaa), wazee wetu wa Zanzibar wametuandalia Dua Maalum ya kuwaombea wachezaji wetu"

"Wazee wetu wanajua kuwa kwa ubora wa timu yetu kwa sasa lazima wenye nia ovu na mbaya na timu yetu wanaweza kutudhuru, Tutasoma Dua kujiepusha na wenye nia mbaya na sisi maana siku hizi ukivaa jezi ya Yanga unaonekana kama unaringa," alitamba Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’