Mshambuliaji Jean Baleke taratibu ameanza kuingia katika mfumo wa kocha Miguel Gamondi na pengine kesho Jumamosi atapatiwa dakika nyingi zaidi katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ethiopia na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Baleke alitumika kwa takribani dakika tano tu
Baleke amekuwa na mwanzo mgumu Yanga pengine ni kutokana na kuchelewa kwake kuanza kuwatumikia mabingwa hao wa nchi sababu ya vibali
Hata usajili wake pia ulichukua muda mrefu kukamilika, akilazimika kusubiri mpaka siku moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa
Katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Baleke alipewa program maalum ya kuzifumania nyavu ikiwa ni dalili pengine anaandaliwa kwa ajili ya kutumika hapo kesho