Kikosi cha Yanga leo kiko visiwani Zanzibar kusaka matokeo ya ushindi katika mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA
Ni katika uwanja wa New Amaan Complex majira ya saa 2:30 usiku Yanga itakuwa ikiwania kuweka rekodi ya aina yake visiwani humo
Wakiwa mbele kwa ushindi wa bao 1-0 ambao waliupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ethiopia wiki iliyopita, sare au ushindi utaihakikishia Yanga kutinga makundi katika ardhi ya Zanzibar
Hadi kufikia jana jioni, asilimia 95% ya tiketi za mchezo huo tayari zilikuwa zimeuzwa, maana yake ni kwamba dimba la Amaan litakuwa 'full house' kuwapa hamasa wachezaji wa YangaΒ
Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wako tayari kusaka ushindi katika mchezo huo ili wafuzu makundi
Wenyewe Wananchi wanasema leo wanaanza rasmi kazi ta kufyeka kichaka cha 'ranking' za CAF ambacho watani zao wamekuwa wakijificha kwa misimu kadhaa
Kila la kheri Wananchi, kila la kheri mabingwa wa nchi....